Search This Blog

Friday, February 7, 2020

Huko VPL ukizubaa unaachwa jumla

By Yohana Challe

MZUNGUKO wa kwanza wa Ligi Kuu (VPL) tayari umetutupa mkono licha ya Namungo FC na Mwadui kuwa na mchezo mmoja wa kukamilisha mzunguko huo. Mengi yameshuhudiwa na sasa tunatarajia kuona mengine katika mzunguko wa pili.

Yapo maamuzi ya utata tumeyashuhudia namna baadhi ya waamuzi wanavyojikoroga, mabao ya lawama, timuatimu ya makocha nayo ilikuwa kama kawaida kwenye ligi hiyo na nyingine za chini yake.

Leo Ijumaa mabingwa watetezi na vinara wa ligi hiyo, Simba wataanza kazi mbele ya JKT Tanzania na michezo mingine ikiendelea kesho katika msako wa alama tatu kwenye viwanja tisa ambako kutawaka moto.

Katika mzunguko wa kwanza baadhi ya mambo ambayo yalijitokeza Mwanaspoti linakuletea kwa karibu japo mengi unayajua mwenyewe ambayo umekutana nayo baada ya kufuatilia timu yako.

WAAMUZI KUBORONGA

Tukiachana na rekodi ambazo jana Alhamisi Mwanaspoti lilieleza namna baadhi ya waamuzi wanavyotoa maamuzi yao kwa kujikanyaga huku wengine wakitofautiana wenyewe kwa wenyewe, juzi Jumatano hali hiyo imeendelea, wakati Azam FC ikiikaribisha Tanzania Prisons katika Uwanja wa Uhuru.

Advertisement

Si hilo pekee, katika mchezo baina ya Yanga na Lipuli FC waamuzi waliingia matatani baada ya maamuzi yao kuwashangaza wengi kutokana na mpira uliodakwa na kipa wa Yanga, Metacha Mnata.

Tayari Rais wa TFF, Wallace Karia ameielekeza Kamati ya Waamuzi kukutana na Bodi ya Ligi kutathmini juu ya mwenendo wa uchezeshaji wa waamuzi na katika kikao hicho watakuwepo baadhi ya maofisa kutoka TFF.

HAT TRICK NNE

Ditram Nchimbi (Polisi Tanzania) sasa yupo Yanga alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat trick wakati timu yake ikitoshana nguvu ya mabao 3-3 dhidi ya Yanga katika Uwanja wa Uhuru kwa mabao yake ya dakika ya 34, 55 na 58.

Mshambuliaji wa Lipuli FC, Darueshi Saliboko alikuwa mchezaji wa pili kufunga hat trick Novemba 7, mwaka jana wakati wakiifunga 5-1 Singida United katika Uwanja wa Samora mjini Iringa kwa mabao yake ya dakika ya 43, 72 na 87.

Obray Chirwa (Azam FC) alikuwa wa tatu kufanya hivyo walipoilaza Alliance FC kwa mabao 5-0 katika Uwanja wa Nyamagana - kwa mabao yake ya dakika ya 4, 25 na 68 huku Kelvin Sabato (Kagera Sugar) naye alipiga tatu walipoilaza 3-0 Singida United Uwanja wa Kaitaba.

Katika michezo 189 ambayo imechezwa mpaka sasa imeshuhudia mabao 375 yakiweka kambani huku, Meddie Kagere (Simba) akiwa kinara kwa mabao yake 12 na Reliant Lusajo (Namungo FC) akiwa na mabao tisa na pointi 513 zimekusanywa.

Simba ndio vinara wa kufunga wakiwa na mabao 42 huku safu yao ya ulinzi ikionekana imara kwa kuruhusu mabao 10 na Singida United sio tu kuwa vibonde wa ligi, pia safu ya ushambuliaji iko butu na ukuta wake sio imara ukiruhusu mabao 28.

WALIOTUPIA KWAO

Katika harakati za kuokoa hatari wachezaji 10 wamejikuta wakijifunga - Ibrahim Said, (Alliance FC) kwenye mchezo dhidi ya Mbao FC wakitoka sare ya bao 1-1, George Chota (Ruvu Shooting) wakati chama lake likibanwa mbavu ya bao 1-1 na Mbeya City, Ally Mtoni ‘Sonso’ (Yanga) wakifungwa 1-0 dhidi ya Azam FC.

Yassin Salum (Polisi Tanzania) bao ambalo lilisababisha timu yake kufungwa 1-0 na Ruvu Shooting, Dickson Daudi (Coastal Union) walipofungwa 2-1 na Mtibwa Sugar, Erick Mrilo (Alliance FC) - bao ambalo liliipa Polisi Tanzania ushindi wa bao 1-0.

Naye Paul Bukaba (Namungo FC) alitupia wakati wakifa nyumbani 3-1 mbele ya Coastal Union, Geofrey Luseke (Alliance) katika ushindi wa 2-1 walioupata mbele ya KMC, Juma Nyosso wakati Kagera ikichapwa 3-1 na Mtibwa Sugar, Michael Ismail (Tanzania Prisons) na kufungwa 2-3 dhidi ya Namungo FC.

MAKOCHA WALIOSEPA

Mpaka sasa makocha 11 wameondoka kwenye timu walizokuwa wakizifundisha mwanzo wa msimu ambao Athuman Bilal ‘Bilo’ (Alliance FC), Amri Said ‘Stam’ (Biashara United), Fred Felix ‘Minziro’ (Singida United), Ndayiragije (Azam FC).

Wengine ni Mlale Hamsini (Ndanda FC), Mwinyi Zahera (Yanga), Jackson Mayanja (KMC), Patrick Aussems (Simba), Seleman Matola (Polisi Tanzania), Juma Mwambusi (Mbeya City) na Herimana Huruma (Lipuli).

MABAO YA MATUTA

Katika mabao 375 yaliyofungwa 18 yametokana na penalti, Meddie Kagere (Simba) amefunga penalti tatu katika michezo dhidi ya Kagera Sugar waliposhinda 0-3, Mbeya City wakipata ushindi wa 4-0 na kwenye sare ya 2-2 mbele Yanga.

David Kameta (Lipuli FC) alifanya hivyo kwenye sare ya 2-2 na Tanzania Prisons, Peter Mapunda (Mbeya City) kwenye ushindi wa 2-1 mbele ya Mbao FC 1-2 na kwenye kichapo cha 2-1 dhidi ya Mwadui FC, Serge Alain (KMC) wakiilaza 2-1 Biashara United na Awesu Awesu (Kagera Sugar) wakishinda 2-1 kwa KMC.

Rajab Zahir (Ruvu Shooting) alifanya hivyo kwenye ushindi wa mabao 2-1 mbele ya JKT Tanzania, Aggrey Morris (Azam FC) dhidi ya JKT Tanzania na kulazimishwa sare ya mabao 2-2, Abdul Hillary (KMC) kwenye sare ya 1-1 na Yanga kisha kwenye kichapo cha 2-1 mbele ya Polisi Tanzania.

Marcel Kaheza (Polisi Tanzania) katika ushindi wa 2-1 dhidi ya KMC, Shaban Idd (Coastal Union) bao ambalo liliwapa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Tanzania Prisons, Sixtus Sabilo (Polisi Tanzania) wakitoa sare ya 1-1 na Biashara United kisha kwenye ushindi wa 2-1 mbele ya Kagera Sugar.

Richard Djodi (Azama FC) wakibanwa 1-1 na Mtibwa Sugar na mwingine ni Ayoub Lyanga (JKT Tanzania) wakati chama lake likilazimishwa sare ya bao 1-1 na Coastal Union.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...