Search This Blog

Tuesday, February 25, 2020

Naibu Waziri wa AFYA Aambukizwa Virusi vya Corona Iran



Naibu Waziri Iraj Harirchi ambaye amekuwa mstari wa mbele nchini humo katika kupambana na #coronavirus amegundulika kuambukizwa virusi hiyo

Msemaji wa Wizara hiyo amethibitisha hayo alipokuwa anafanya mahojiano na chaneli ya runinga ya Taifa na kusema Naibu Waziri huyo amewekwa sehemu maalumu ya uangalizi

Aidha, Jumatatu iliyopita Shirika la Habari nchini humo lilisema watu 50 wamefariki kwa virusi hivyo huku likieleza kuwa linapendelea kutokuficha mambo kuhusu Corona kwani yanahusisha maisha ya watu

Hata hivyo, Naibu Waziri Harirchi alipinga taarifa hiyo akisema atajiuzulu ikiwa hata nusu ya idadi iliyotajwa (Watu 50) watafariki dunia kutokana na Virusi vya Corona

Taarifa kutoka Ikulu zilithibitisha maambukizi ya kwanza ya Virusi vya Corona nchini humo Jumatano iliyopita huku Wizara ya Afya ikisema watu wawili wameambukizwa na wametengwa


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...