Search This Blog

Monday, February 17, 2020

Mnaigeria Aliyepata Umaarufu DUNIA Nzima Kwa Picha yake ya Kulia


Anaitwa Oladee kijana mzaliwa wa Nigeria. Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Ilorin nchini Nigeria

Mwaka 2009 Oladee alipata mkasa mkubwa ambapo baadaye mkasa huo ukamfanya kuwa mtu maarufu. Alipewa Naira 200 sawa na Tsh. 1,200 na bibi yake kununulia mahitaji ya chakula

Aliongozana na rafiki yake aliyemshawishi acheze Kamari. Hela yote aliyopewa ikaliwa kwenye kamari (bet), hapo bwana Oladee alipoanza kulia ili arudishiwe hela yake

Walimpiga picha na kichwa chake kinatumika kwa kupachikwa kwenye picha tofauti tofauti za kuchekesha

Watu wanamwita kichwa kinachotembea bila 'passport' kwa sababu picha yake hii imesambaa Dunia nzima na watu wanaihariri ‘edit’ kwa kuifanyia vituko

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...