Search This Blog

Wednesday, February 5, 2020

Mbunge Lulida awapiga jeki waathirika wa mafuriko Lindi

Na Ahmad Mmow, Lindi

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Lindi   Riziki Lulida amekabidhi  msaada wa chakula  tani 4 , vyandarua 500  na  maturubai 200  kwa waathirika wa mafuriko katika vijiji  vya Nanjima  A  , na Nanjima B jimbo la mchinga mkoani Lindi.

Akizungumza na Wananchi wa viijiji hivyo  wakati akikabidhi misaada hiyo, alisema ameguswa na madhara  mafuriko ambayo licha ya kusababisha watu wakose makazi, lakini pia yamepoteza  uhai wa watu na mali zao. Kwahiyo ameona umuhimu wa kutoa misaada ili  kuwasaidia waathirika waliopoteza ndugu na  mali  zao wakati wa mafuriko.

Alisema ametoa   msaada huo kwa jamii   iliyokumbwa  na maafa   baada ya kutembelea baadhi ya maeneo ya waathirika waliokumbwa na mafuriko Lindi vijijini .ikiwemo Kitomanga na Nangaru.

“Mimi  mbunge wenu  wa viti maalumu   nimetoa msaada wa  chakula, marutubai na vyandarua  kwa sasa lakini wakati  bado nitaendelea kuwaunga mkono serikali, nitahakikisha tunaendelea kushirikiana katika wakati huu wa shida na wakati wa raha  na nyakati zote. Tupo pamoja, nitawahudumia," alisema Lulida.

 Mbunge huyo alisema juhudi za makusudi zinahitajika  katika  kipindi hiki kigumu kutokana na waathirika kuhitaji misaada ya kijamii baada ya kukumbwa na  hayo yaliyosababisha wapoteze makazi ,vyakula , mifugo na   mazao  yao.

 Mmoja wa athirika hao, Baraza Maduhu  mkazi wa  kijiji cha Kitomanga akizungumza kwanianiaba ya wanakijiji wenzake licha ya  kumshukuru mbunge  huyo na serikali kwa kutoa misaada mbalimbali alisema wanatunaimani itawasaidia na kujipanga upya kuendesha familia zao.
.
Lakini pia, Maduhu aliiomba serikali iwapatie maneo mengine ili waache kuishi mabondeni. Ambapo mvua kubwa ikinyesha maji hujaa mtoni na kuingia ndani kusababisha mafuriko.

Kwaupande wake mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga alisema  mbunge huyo ameonesha moyo wa  kuthamini jamii yenye matatizo  kwa kujali janga la mafuriko ambalo limeathiri  kwa kiasi kikubwa shughuli za maendeleo. Huku  akiwaomba wadau wengine kuiga mfano huo.

Alisema kunahitaji sana misaada,kama  ya chakula,  nguo na dawa. Kwani mpaka sasa kuna kambi nne zenye watu zaidi 843 waliokumbwa na mafuriko Lindi vijijini.

 Alisema serikali  imetenga maeneo ya  viwanja ambavyo vitagawiwa kwa wananchi wote waliokumbwa na mafuriko ili wakaendelee na shughuli zao za kiuchumi na maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...