Search This Blog

Wednesday, February 5, 2020

Vikwazo kwa Wahandisi wenye leseni zilizokwisha muda wake


Na James Timber, Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amewataahadharisha wahandisi watakaokuwa na leseni zilizoisha muda wake kuwa hawatapata nafasi ya kufanya kazi mkoa wa Mwanza kuanzia April Mwaka huu.

Mongella amewataka wahandisi kuwa na leseni ambazo hazijaisha muda wake hivyo wote wenye leseni zilizoisha muda wanatakiwa kulipia leseni mpya zoezi ambapo mwisho ni 31, Machi mwaka huu na baada ya hapo atazungumuza na wakuu wa wilaya wote wasifanye kazi na mhandisi ambaye hana vigezo hivyo.


"Serikali yetu toka imeingia madarakani imetoa kipaumbele kwa wahandisi wazawa kwa kuwa inaamini nyinyi ndio mnaweza kulifikisha taifa katika uchumi wa viwanda pasipo kikwazo chochote.

"Lakini naomba mtambue kuwa ili mhandisi uweze kuaminika na kupewa kazi bila kutiliwa shaka lazima uwe na leseni iliyohaishwa kwa maana ya ile ambayo inatambulika na mamlaka husika, hivyo nami kama kiongozi wa mkoa niwaambieni nitafanya kazi na wenye leseni zilizo ndani ya matumizi tu na si vinginevyo.

"Binafsi napenda kufanya kazi na kila mhandisi aliyekizi  kigezo kwa maana hiyo sitegemei baada ya muda wa mwisho wa kuhaisha leseni nilioutoa kuisha niwaambie kabisa hakuna mhandisi mwenye leseni iliyoisha muda wake atafanya kazi kwenye mkoa wangu.

"Pia niwakumbushe kuwa kazi ya uhandisi kama mnavyojua ni kazi ya kiapo ndio maana leo pia kuna wenzenu wamekula kiapo hii ni ishara kuwa kazi yenu inabeba roho za watu na inategemewa hivyo jitahidini kufanya kazi kwa kuzingatia kiapo chenu ili kazi yenu iwe na manufaa kwa taifa lenu na si vinginevyo hasa katika kipindi hiki cha Sera ya Tanzania ya viwanda," amesema Mongella.

Aidha awali akisoma taarifa ya utangulizi, Msajili kutoka Bodi ya Usajili ya Wahandisi Tanzania (ERB) Mhandisi Patrick Barozi amesema kuwa hadi sasa kuna jumla ya wahandisi waliosajiliwa 26,618 nchi nzima ambapo miongoni mwao wahandisi 2925 ni wanawake sawa na asilimia 21.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...