Search This Blog

Thursday, February 6, 2020

Mbeya: Diwani wa CHADEMA acharangwa mapanga


Diwani wa Kata ya Isesye, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Mbeya Ibrahim Mwampwani, amecharangwa mapanga usoni na kichwani na watu wasiojulikana.

 Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama hicho, John Mrema, amesema kuwa diwani huyo tayari amekwishatoa taarifa Polisi na kwamba baada ya tukio lile alipelekwa hospitali na sasa amesharuhusiwa na anaendelea vizuri.

"Ilikuwa jana usiku wakati anatoka kwenye shughuli zake, akavamiwa na watu kama watano wakamjeruhi paji la uso na kichwani, ametibiwa na kesharuhusiwa na hawakumuibia chochote, tukio limetokea karibu na nyumbani kwake, yeye nimeongea naye analihusisha tukio hili na masuala ya kisiasa" amesema Mrema.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...