Search This Blog
Thursday, February 6, 2020
Familia ya wasomi wa CCM Kigoma wamvaa Zitto Kabwe
Familia ya wasomi wa Chama cha mapinduzi(CCM) mkoani kigoma wanazuoni wametoa tamko juu ya kitendo alichokifanya mbunge wa kigoma mjini mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe cha kupeleka maombi ya zuio la mkopo kwa serikali ya Tanzania bank kuu kwaajili ya kuboresha Elimu.
Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Mkoa za chama cha mapinduzi wanazuoni hao wamesema kuwa jambo alilolifanya Zitto halikubaliki na ni kitendo kisichoungwa mkono kabisa na wanakigoma na hakipaswi kuigwa na mtu yeyote.
"Kitendo alichokifanya Zitto siyo kitendo kizuri kwasababu Zitto ni mbunge kwani ana uwanja mkubwa wa kuzungumza hayo bungeni nasiyo kuandika barua binafsi yeye kama zitto ya kuzuia fedha za mkopo wa kuboresha elimu toka bank kuu"alisema Eliya Michael mwana CCM na mwanazuoni wa Mkoa wa Kigoma
Eliya alisema kuwa Zitto anapaswa kukemewa kwa jambo alilolifanya kukaa kimya watu wataona jambo alilolifanya ni sahihi lakini wao kama wanakigoma wanasema alichokifanya zitto hakipaswi kuigwa na mtu yeyote.
Naye William Mtula mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa alisema kuwa hivi sasa ni wakati wa watanzania kuungana pamoja na kumtia moyo Rais kwa kazi kubwa na nzuri anazozifanya za kuwaletea maendeleo wananchi.
Mtula alisema kuwa matakwa ya Watanzania nikupata huduma bora na za msingi kama vile elimu,afya,miundombinu na zingine.
"Zitto ni mbunge pia ni mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Kigoma mjini bungeni hivyo alipaswa kuongelea hoja za wananchi wake na kero zilizopo jimboni kwake na sihayo aliyoyafanya dhidi ya serikali yake"alisema
Wanazuoni hao wamewataka wananchi wa jimbo la Kigoma mjini kulitafakari hilo na kuona sasa ni wakati wao wa kutafuta mwakilishi ambaye atawawakilisha vizuri na siyo yule anayefanya kazi amabazo wananchi hawajamtuma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment