Search This Blog

Sunday, February 9, 2020

Manchester United yampa presha Cantona

London, England. Nguli wa zamani wa Manchester United Eric Cantona amesema ana hofu mashabiki wa klabu wataacha kutaja jina lake uwanjani.

Mashabiki wa Man United wanamuona Cantona ni mchezaji mwenye mafanikio baada ya kuiongoza vyema alipokuwa nahodha.

Licha ya kuondoka Man United miaka 23 iliyopita baada ya kustaafu soka akiwa na kiwango bora, Cantona amekuwa akihusudiwa zaidi na mashabiki wa klabu hiyo.

Mashabiki wa klabu hiyo wamekuwa wakilitaja jina lake katika mechi za timu hiyo jukwaani sanjari na kuweka mabango ya picha zake.

Katika kipindi cha miaka minne na nusu aliyocheza Man United chini ya Sir Alex Ferguson, Cantona (53) aliipa mataji manne ya Ligi  Kuu na mawili ya Kombe la FA.

“Najivunia, naona fahari lakini nina hofu ipo siku mashabiki wataacha kutaja jina langu,”alisema nguli huyo.

Advertisement

Kauli ya Cantona imekuja kipindi ambacho Man United haifanyi  vizuri katika mechi za mashindano mbalimbali tangu alipostaafu Ferguson mwaka 2013.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...