Search This Blog

Sunday, February 9, 2020

Bayern Munich yamuwekea donge nono Firmino

Munich, Ujerumani. Bayern Munich imetenga Pauni75 milioni kunasa saini ya mshambuliaji nyota wa Liverpool Roberto Firmino.

Bayern imekuwa klabu ya kwanza kutangaza dau kwa Mbrazili huyo ikimtaka katika usajili wa majira ya kiangazi.

Klabu hiyo imesema iko tayari kutoa dau hilo kumsajili Firmino ambaye amekuwa kinara wa mabao Liverpool.

Licha ya kumwania mshambuliaji huyo, klabu hiyo inaendelea na mpango wake wa kumsajili winga wa Manchester City Leroy Sane.

Winga huyo wa Ujerumani ndio chaguo la kwanza kwa klabu hiyo na ilipanga kumsajili katika dirisha dogo kabla ya mpango huo kukwama.

Bayern Munich inamtaka Firmino kujaza nafasi ya mshambuliaji nguli Robert Lewandowski.

Advertisement

Firmino (28) ambaye ni mshambuliaji asilia anatajwa kuwa hodari wa kufunga kama alivyo Lewandowski. Mkataba wa nyota huyo Anfield unamalizika mwaka 2022.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...