Search This Blog

Wednesday, February 26, 2020

Kobe na machozi ya Michael Jordan

By Matereka Jalilu

KABLA ya kwenda kwake katika kumbukumbu maalum ya kuwaaga Kobe Bryant na mwanaye Gianna miongoni mwa watu saba waliofariki pamoja kwenye ajali ya helikopta mwezi mmoja uliopita, Michael Jordan alishindwa kujizuia kulia licha ya ahadi ya kutolia tena.

Ipo hivi, Michael Jordan ambaye ni gwiji wa mchezo wa kikapu Marekani (NBA), aliwahi kuteka mtandaoni miaka kumi nyuma kwa picha yake akiwa analia kwa huzuni hadi kusababisha kuwepo kwa neno maalum lililoitwa “Crying Jordan” ambapo kulia kwake kwa mara nyingine anahofia kurudi kwa kibonzo hicho.

Neno hilo lilitumika kwa muda mrefu hadi aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama kumsisitizia Jordan mwenyewe kuwa ni zaidi ya ilivyo kwenye muonekano uliopo kwenye mtandao wakati akimpatia tuzo mwaka 2016 huku yeye mwenyewe kuna wakati huwa anajiona ndani ya vibonzo hivyo!

Imekuwaje? Ni siku hiyo ya kumbukumbu ya Kobe na Gigi iliyofanyika katika uwanja wa Staples Center wa timu ya Los Angeles Lakers aliyocheza muda wote wa miaka 20, ambapo Michael Jordan alishindwa kuzuia kulia kwake wakati akizungumza na kufichua kuwa alimuahidi mkewe kuwa hatolia kwa miaka mitatu au minne ijayo lakini kifo cha Kobe kimeshindwa kulinda ahadi yake kwani ilikuwa ni lazima alie kwa uchungu wa kufariki kwake.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...