
Kilimanjaro. "Simba....Simba...Simbaaa" ndivyo maelfu ya mashabiki waliofurika katika mbio za Kilimanjaro marathoni walimshangilia afisa habari wa klabu hiyo, Haji Manara kwenye viwanja vya Ushirika mjini Moshi wakati akimaliza mbio.
Manara ameshiriki mbio za msimu huu na kukimbia na kumaliza mbio kilomita 22 alipotumia saa 1.54 kumaliza.
Wakati msemaji huyo wa Simba akihitimisha mbio hizo, mashabiki walisimama kumshangilia wakiimba Simba Simbaaaa Simbaaa, klabu inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara na bingwa watetezi wa Ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment