Search This Blog

Wednesday, February 19, 2020

Bongo Zozo ala shavu Jingine

By Thomas Ng'itu


SIKU chache tangu ateuliwe kuwa, Balozi wa Maliasili na Utalii, shabiki maarufu wa Taifa Stars, Nick Reynolds ‘Bongo Zozo’ amelamba shavu jingine la kuwa balozi katika klabu ya Lipuli FC.

Bongo Zozo jana (Jumatano) akiwa katika ofisi za Lipuli mkoani Iringa, alitangazwa kuwa balozi wa klabu hiyo na kuanza kazi mara moja ya kuhamasisha mashabiki wazidi kuipenda timu hiyo.

Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Iringa, Bongo Zozo alisema amefurahishwa na uteuzi huo uliofanywa na Wanapaluhengo akidai amevutiwa nao zaidi kuliko angepewa wa klabu kubwa nchini.

“Nimekuwa nikipenda kushangilia timu ndogo siku zote ndio maana imekuwa rahisi kuwa na mapenzi na Lipuli, nilivyokuja Tanzania nilikaa na kutafuta maisha mkoani Iringa,’’ alisema.

Aliongeza kwa kusema; “Waliponitafuta na kutaka niwe balozi sikuona sababu ya kukataa, nipo tayari kufanya fujo zisizoumiza,” alisema raia huyo wa Uingereza ambaye amekuwa bega kwa bega kuipiga tafu Taifa Stars na kumshangilia Mbwana Samatta ndani ya timu yake ya Aston Villa.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...