Klabu ya Yanga Sc imetangaza usajili wa mchezaji raia wa Ghana, Bernard Morrison mwenye umri wa miaka 26, kutoka klabu ya DC Motema Pembe ya nchini DRC Congo.
Takwimu za Morrison: Ligi kuu Afrika Kusini amecheza michezo 18 na kufunga mabao mawili, ligi kuu Ghana katika michezo 16 ametikisa nyavu mara 6.
Mchezaji huyo anamudu kucheza nafasi mbalimbali uwanjani katika safu ya ushambuliaji, mshambuliaji wa kati na mshambuliaji wa pembeni akitokea kulia ama kushoto.
Bernard amewahi kuchezea timu kadhaa kabla ya kutua Jangwani katika dirisha hili dogo la usajili, amepita As Vita, Dc Motema Pembe, Ashanti ya Ghana na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment