Na Amiri kilagalila-Njombe
Wakati mwaka huu 2020 Tanzania ikitarajia kuwa na uchaguzi mkuu wa kuwachagua wabunge,madiwani na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania taasisi ya kuizuia na kupambana na rushwa mkoani Njombe (takukuru)imesema ,tayari imejipanga vilivyo kukabiliana na vitendo mbalimbali vinavyoashiria rushwa ndani ya jamii ili kuhakikisha viongozi watakaochaguliwa hawatopatikana kwa rushwa.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari,kaimu kamanda wa takukuru mkoa wa Njombe Noel Mseo amesema taasisi itafanya kazi kwa mujibu wa sheria kuhakikisha inazuia vitendo vyote vya rushwa katika uchaguzi huo na hata katika chaguzi nyingine kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya rushwa katika maendeleo.
“kama takukuru hatusubiri tunaanza kufuatilia vitendo vya rushwa,pale tu michakato ya uchaguzi itakapoanza,kwa hiyo tunaangalia na tunafuatilia michakato yote inayoendelea hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu wakati wa kipindi cha uchaguzi mkuu”alisema Noel Mseo
Baadhi ya wananchi akiwemo Dastan Mkongwa na Lunogelo Mgimba wameitaka taasisi hiyo kuhakikisha kuwa viongozi wanaokamatwa na makosa ya rushwa wanashughulikiwa ipasavyo na vyombo vinavyohusika ili kuondoa rushwa katika chaguzi mbalimbali.
Aidha kaimu kamanda huyo amesema kuwa taasisi hiyo kwa kushirikiana na kamati maalumu iliyoundwa na mkuu wa mkoa wa Njombe kwaajili ya kukusanya madeni ya vyama vya ushirika na Njocoba kutoka kwa wadaiwa sugu, itaendelea kushirikiana kufuatialia madeni hayo huku wadaiwa ambao hawajafikiwa wakitakiwa kujitokeza haraka iwezekanavyo.
“Hadi kufikia tarehe 13 mwezi wa kwanza 2020 tumefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni mia tisa arobaini na saba,mia tatu tisini na mbili milioni na mia nane thelathini na nne na sifuri point inane.Kazi ya kukusanya madeni haya sugu inaendelea lengo la serikali hii ya awamu ya tano ni kuhakikisha rasimali za wananchi ambazo zinaelekea kupolwa na watu wachache zinaludi kwa wananchi wenyewe”alisema Noel Mseo
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment