
London, England. Nani anamtaka Pierre-Emerick Aubameyang kama una wachezaji chipukizi ambao wanasisimua uwanjani.
Nahodha huyo wa Arsenal atarejea uwanjani Jumamosi wiki hii kuikabili Burnley baada ya kukamilisha adhabu ya kufungiwa mechi tatu.
Mshambuliaji huyo alipewa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace.
Arsenal sasa ina chipukizi wawili Bukayo Saka na Eddie Nkatiah ambao jana walifanya mambo makubwa katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Bournemouth.
Saka (18) na Nkatiah (20) kila mmoja alifunga bao na kuchangia ushindi wa mabao 2-1 iliyopata Arsenal katika mchezo huo.
Arsenal imecheza mechi 10 bila Aubameyang msimu huu ambaye Barcelona inamtaka kwenda kuziba pengo la Luis Suarez ambaye atakuwa nje ya uwanja miezi mitatu baada ya kuumia.
Arsenal inamtegemea nyota huyo mwenye thamani ya Pauni56 milioni, lakini kocha Mikel Arteta anaweza kushusha presha endapo chipukizi hao wataendeleza moto.
No comments:
Post a Comment