Search This Blog

Monday, January 27, 2020

NBA yafuta mechi ya Los Angeles Lakers

Los Angeles, Marekani. Los Angeles Lakers itacheza na Portland Ijumaa wiki hii baada ya mechi yake dhidi ya Clippers kuahirishwa.

Shirikisho la Mpira wa Kikapu Marekani liliahirisha mechi hiyo kufutia kifo cha aliyekuwa mchezaji nyota wa Los Angeles Kobe Bryant kufariki.

Kobe alifariki katika ajali ya helikopta akiwa na mwanaye Gianna na watu wengine saba Jumapili iliyopita.

Taarifa ya shirikisho hilo ilisema uamuzi huo umefikiwa ili kutoa nafasi kwa Lakers kuomboleza kifo cha nguli huyo.

LeBron James na wachezaji wengine wa Lakers walitoa machozi baada ya kupata taarifa za Kobe anayetajwa kuwa mmoja wa wachezaji bora wa mpira wa kikapu waliowahi kutokea duniani.

Kwa mara ya kwanza Lakers, imetoa taarifa inayosema: "Los Angeles Lakers inawashukuru wote kwa kuungana nasi katika maombolezo haya.

Advertisement

“Tunapitia kipindi kigumu wote, tunaendelea kuungana na familia ya Brynt na tutatoa taarifa zaidi,”ilisema taarifa ya klabu hiyo.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...