Search This Blog

Monday, January 27, 2020

Man United yamgeuzia kibao Sanchez

London, England. Manchester United imemtaka Alexis Sanchez kuthibitisha ubora wake Old Trafford huku kukiwa na taarifa za klabu hiyo kutaka kumrejesha.

Mshambuliaji huyo anayelipwa mshahara wa Pauni500, 000 kwa wiki, amepelekwa kwa mkopo Inter Milan ya Italia.

Man United inasita kumpiga bei Inter Milan na klabu hiyo imepanga kumpa nafasi nyingine ili kuthibitisha ubora wake Man United.

Mchezaji huyo mwenye miaka 31, anatarajiwa kuwemo katika kikosi kitakachokwenda Marekani kwa maandalizi ya msimu mpya wa majira ya kiangazi.

Licha ya kupelekwa Inter Milan baada ya kukosa namba Man United, Sanchez anapambana na majeraha ya mguu ingawa aliingia akitokea benchi katika mchezo waliotoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Cagliari mwishoni mwa wiki.

Sanchez bado anamiliki jezi namba saba Man United na amebakiza miaka miwili kabla ya mkataba wake kumalizika.

Advertisement

Sanchez alitua Man United Januari 2018 akibadilisha na Henrikh Mkhitaryan aliyekwenda Arsenal. Hata hivyo, mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile alishindwa kutamba na kufunga mabao matano katika mechi 45 alizocheza.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...