Kamishina Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Ilala, Janeth Magomi, amethibitisha kifo cha Mwandishi wa Habari, Deogratius David, aliyekutwa amefariki Dunia chumbani kwake, maeneo ya Vingunguti Mji Mpya, huku mwili wake ukiwa umeharibika vibaya.
Kamanda Janeth amesema kuwa, taarifa walizipata kutoka kwa majirani, baada ya kupita siku tatu bila kumuona na kusikia harufu kali ikitoka chumbani mwake na ndipo walipoamua kuvunja mlango.
"Mwili wake ulikutwa umelala kifudifudi kitandani kwake ukiwa umeharibika tayari, majirani wanasema waliamua kuuvunja mlango baada ya kutomuona kwa siku tatu, lakini pia kusikia harufu iliyokuwa ikitokea chumbani mwake na wanasema marehemu alikuwa na ugonjwa wa kifafa" amesema ACP Magomi.
Mwili wa marehemu Deoglatius umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment