Search This Blog

Wednesday, January 8, 2020

Mila na desturi vyatumika kama kichaka cha kufichia ukatili wa kijinsia Newala

Na Ahmad Mmow, Newala.


Mila na desturi vimetajwa kutumika kama vichaka vya kufichia vitendo vya ukatili wa kijinsia na baadhi ya watu, hasa wanaume wanaotenda vitendo hivyo katika halmashauri ya Newala, mkoa wa Mtwara.

Hayo yameelezwa na mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii ya halmashauri ya wilaya ya Newala, mkoa wa Mtwara, Christina Kambuga. Alipozungumza na Muungwana Blog mjini Newala, baada ya kuulizwa kama kuna vitendo vya ukatili wa kijinsia katika eneo la halmashauri hiyo, na ushirikiano wa idara yake na  kituo cha msaada wa kisheria na haki za binadamu wilayani Newala( PCO).

Kambuga alisema vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji ni miongoni mwa vitendo ambavyo vipo katika halmashauri hiyo na wilaya ya Newala kwa jumla. Huku kundi kubwa la waathirika wa vitendo hivyo akilitaja kuwa ni wanawake. Hata hivyo watu wengi hawatoi taarifa wanapotendewa au wanapoona vitendo hivyo vikifanyika.

" Wanaotendewa wanaona wanatendewa haki. Wanaamini kwamba ukatili wanaotendewa ni haki yao kwamujibu wa mila na desturi. Mwanamke anaweza kufukuzwa bila kupewa chochote na mume wake lakini hasemi, ananyanyaswa hasemi," alisema Kambuga.

Alisema kutokana na. ukweli huo baadhi ya watu, hasa wanaume wanatenda vitendo hivyo dhidi ya wanawake bila hofu. Huku wakijiona wanahaki ya kutenda vitendo hivyo kwani mila na desturi zimewapa uwezo wa kufanya hivyo. Huku wanaotendewa wakiungana na mtazamo huo hasi kwao..

Alisema hali hiyo inasababisha kutopokelewa taarifa nyingi za vitendo hivyo kwenye ofisi za maendeleo ya jamii, madawati ya kijinsia na vituo vya misaada ya kisheria. Kwani hata watu wengi wanaoona vitendo hivyo vikifanywa, hawawafichui wanaotenda. Kwani wanaona nikawaida tu.

Aidha Kambuga alisema idara yake ina ushirikiano mkubwa na PCO katika utatuzi na usuluhishi wa migogoro katika jamii wilayani humo. Hata hivyo alitoa wito kwa vituo na mashirika ya misaada ya kisheria na haki za binadamu yatangaze  shughuli zake kupitia vyombo vya habari badala ya kutegemea mikutano na matamasha pekee.

Kuhusu halmashauri hiyo inashirikije kutoa elimu inayohusu ukatili wa kijinsia na ukiukwaji wa haki za binadamu, Kambuga alisema imekuwa ikitekeleza wajibu huo wa msingi kwa jamii kwa kadiri ya uwepo wa raslimali zinazoweza kusababisha jamii kufikiwa na kupewa elimu. Hasa raslimali fedha.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...