Search This Blog

Tuesday, January 7, 2020

Mane mchezaji bora Afrika

London, England. Mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika 2019.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal alishinda tuzo hiyo baada ya kumpiku mchezaji mwenzake wa Liverpool, Mohamed Salah raia wa Misri na winga wa Manchester City na Algeria Riyad Mahrez.

Mane (27) aliisaidia Liverpool kutwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 2018-2019 akifunga mabao 30 katika mechi za mashindano mbalimbali.

Pia alifunga mabao 15 msimu 2019-2020 na kuipa Liverpool pointi 13 katika msimamo wa Ligi Kuu England.

“Nina furaha kubwa kushinda tuzo hii. Mpira ni kazi yangu, naupenda. Napenda kuishukuru familia yangu, wachezaji wenzangu wa timu ya taifa, shirikisho na klabu ya Liverpool, leo ni siku yangu,”alisema Mane.

Wakati hafla ya utoaji tuzo ikifanyika Hurghada, Misri, Salah aliyetwaa tuzo hiyo miaka miwili iliyopita na Mahrez hawakutokea katika tukio hilo.

Advertisement

Miaka mitatu iliyopita Mane alishika nafasi ya tatu. Mane anakuwa mchezaji wa pili Senegal kutwaa tuzo hiyo nyuma ya nahodha wa zamani wa timu hiyo El Hadji Diouf, aliyotwaa mwaka 2002.

Salah, Mane na Mahrez wamejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 11 wa Afrika wakiungana na nyota watatu wa Ligi Kuu England Joel Matip, Serge Aurier na Pierre-Emerick Aubameyang.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...