Search This Blog

Saturday, January 11, 2020

Maandamano yaibuka kulaani kuangushwa ndege ya abiria Iran



Maandamano makubwa yameripotiwa usiku wa Jumamosi kwenye maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Iran Tehran, baada ya nchi hiyo kukiri kuwa kombora la kijeshi liliiangusha ndege ya abiria ya Ukraine.

Mamia ya watu wameshiriki maandamano hayo ya usiku kuikosoa serikali ya nchi hiyo na hatua yake ya hapo kabla ya kupinga madai kuwa kombora lilikuwa chanzo cha ajali hiyo.

Kulingana na shirika la habari la Isna waandamanaji nje ya chuo kikuu cha Amir Kabir wametaka wote waliohusika na kuangushwa ndege hiyo wajiuzulu.. Wakati huo huo rais Donald Trump wa Marekani ameionya Iran dhidi ya kujaribu kufanya ukandamizaji wa maandamano hayo na kutoa wito kwa nchi hiyo kuruhusu makundi ya haki za kirai kufuatilia kile kinachoendelea.

Ujumbe wa Trump umekuja baada ya polisi kuwatawanya wanafunzi waliokuwa wakitoa kauli kali kuwakumbuka wahanga wa ajali ya ndege iliyotokea Jumatano iliyopita.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...