KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji Sven Vanderboeck ametamba kwamba atawashushia kipigo wapinzani wake Mwadui FC ambao anacheza nao leo Jumamosi kwa kuwa tayari ameshalijua soka la Bongo.
Kocha huyo ametamba kuwa atawashushia kipigo Mwadui FC ambao wanacheza nao kwenye Kombe la Shirikisho (FA) kwa sababu ametambua timu nyingi za hapa nchini zinatumia mfumo wa mipira mirefu.
Kocha huyo amesema kwamba ameshajua mbinu hiyo ya wapinzani wake, ndiyo maana kwa sasa anapata ushindi katika mechi zake zote za ligi na michuano hiyo mingine.
“Kwa sasa nimekaa hapa Bongo nimeshatambua kwamba timu nyingi zinacheza kwa kutumia mfumo mmoja, wanatumia mipira mirefu na karibu wote wanalingana kwa kutumia staili hiyo.
“Nimeshatambua kwa sasa ndiyo maana unaona tunapata ushindi katika mechi zetu, kwa sababu ninapanga watu ambao wana uwezo wa kukimbia pale ambapo wanapocheza hivyo.
“Tulipata ushindi kwenye mechi zetu zilizopita kule Mwanza na hiyo inatupa nguvu ya kufanya vizuri katika mechi zetu zote ambazo zinakuja,” asema Mbelgiji huyo.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment