Mkutano maalumu wenye ajenda ya kupokea taarifa ya timu iliyochunguza tuhuma dhidi Meya wa Jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania, Isaya Mwita utafanyika leo Alhamisi Januari 9, 2020 saa 4 asubuhi katika ukumbi wa Karimjee.
Awali kulikuwa na taarifa zinazoeleza huenda mkutano huo maalumu usifanyike badala yake utafanyika kesho Ijumaa kutokana na Mwita kwenda Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kuweza zuio la kutojadiliwa katika kikao chochote kitakachoitishwa.
Hata hivyo, uamuzi huo wa Mahakama unatarajiwa kutolea leo Alhamisi na Hakimu wa Mahakama hiyo, Janeth Mtenga wa kukubali ombi la Meya Mwita au wajibu maombi ambao ni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mwita anaomba zuio hilo ili kusubiri hadi kesi ya msingi aliyoifungua mahakamani hapo itakaposikilizwa.
Jana Jumatano wajumbe wa Baraza hilo walipewa taarifa za kutokuwapo kwa kikao hicho kilichokuwa kimeitishwa juzi na Mkurugenzi wa Jiji hilo, Sipora Liana hadi kesho Ijumaa Januari 10, 2020 lakini ilipofika usiku, walipigiwa tena simu wakitaarifiwa uwepo wa kikao hicho.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment