Search This Blog

Thursday, January 2, 2020

Gari la mafuta lateketea kwa moto na kujeruwi wawili Mbeya


Gari lenye namba za usajili T. 956 DRT/T. 886 DRV aina ya Scania Tanker la Mafuta mali ya kampuni ya “world oil” lililokuwa limepakia mafuta aina ya Petroli kutokea Dar es salaam kuelekea nchini Zambia limeteketea kwa moto na kujeruhi watu wawili na kusababisha uharibifu wa mali.

Gali hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva ISSA YUSUPH [35] mkazi wa Jijini Dar es Salaam lilipata hitilafu za kiufundi siku ya tarehe 01/01/2020 majira ya saa 16:30 jioni na baadae liliungua moto na kuteketea wakati wa harakati za kufaulisha mafuta kwenye gari hiyo kwenda kwenye gari namba T 844 AWJ Trailer

Watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo ya moto JULIUS DAUDI [30] pamoja na STANFORD MWAKYUSA [45] wote wakazi wa Igurusi Wilayani mbarali.

Aidha katika ajali hiyo kulitokea uharibifu kwa gari namba SM 4633 aina ya Isuzu mali ya Jeshi la Zimamota na Uokoaji na gari namba T 844 AWJ Trailer.

 Chanzo cha ajali ni mlipuko uliotokea kwenye mashine ya kufaulishia mafuta aina ya “water pump”. Majeruhi wamekimbizwa kituo cha afya igurusi kwa matibabu.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...