Search This Blog

Wednesday, January 29, 2020

Courtois anawafunga midomo waliomponda

MADRID, HISPANIA . KIPA wa Real Madrid, Thibaut Courtois anazidi kuwafunga midomo watu waliokuwa wanaponda uwezo wake baada ya kutua Santiago Bernabeu akitokea Chelsea, kutokana na kiwango kikubwa anachokionyesha katika siku za karibuni.

Baada ya kuanza kwa kusuasua maisha yake ndani ya Real Madrid, katika siku za karibuni Courtois amekuwa na kiwango cha juu sana akiruhusu mabao matatu katika mechi 11 za mwisho. Katika mechi 11 za mwisho Mbelgiji huyo pia amecheza mechi nane bila kuruhusu nyavu zake kuguswa. Ni Valencia, Sevilla na Real Sociedad ndiyo zimefanikiwa kumtungua Courtois katika kipindi hicho.

Kipa huyo ameruhusu mabao sita katika mechi 16 za mwisho za michuano yote, katika kipindi hicho alicheza mechi tano mfululizo za Ligi bila nyavu zake kuguswa na huu ni ushahidi tosha kuwa kwa sasa yeye ndiye ukuta kwenye lango la Madrid.

Real Madrid ndiyo timu iliyocheza mechi nyingi kati ya zote katika ligi tano kubwa Ulaya bila kuruhusu mpinzani kupiga shuti hata moja langoni kwake - dhidi ya Sevilla ugenini, Osasuna nyumbani na Real Valladolid ugenini.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...