Search This Blog

Wednesday, January 29, 2020

BARCELONA imesisitiza inataka kumsajili kinara wa mabao wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang.

Miamba hiyo ya La Liga inasaka mshambuliaji baada ya straika wake namba moja Luis Suarez kuwa majeruhi na inamuona Aubameyang ni mtu mwafaka wa kumsajili kabla ya dirisha halijafungwa kesho Ijumaa.

Aubameyang mwenye mabao 16 Arsenal katika michuano yote msimu huu bado hajasaini dili jipya la kubaki Emirates, jambo linalowapa wakati mgumu mabosi wake wakiwa na wasiwasi ataondoka.

Wasiwasi wa Barca Arsenal inaweza kumthaminisha Aubameyang na Pauni 50 milioni, kiwango cha pesa ambacho haitakuwa tayari kukilipa kwa mchezaji ambaye amebakiza miezi 18 tu mkataba wake kufika mwisho.

Lakini, inajipa matumaini Aubameyang anataka kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, hivyo atalazimisha tu dili hilo litokee. Jambo hilo litaleta mvutano kwani Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta naye hataki kumwaachia Aubameyang aondoke licha ya kuibuka kwa Gabriel Martinelli.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...