NEWCASTLE, ENGLAND . SHIRIKA la Kimataifa la Haki za Binadamu, Amnesty International, limeitaka dunia kutambua kuwa Saudi Arabia inatumia michezo kuusahaulisha Ulimwengu juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na taifa hilo.
Hii inakuja baada ya kuwa na taarifa kuwa Mwana Mfalme, Mohammed Bin Salman anataka kutumia taasisi yake ya Saudi Arabian Sovereign Wealth Fund, kuinunua klabu ya Newcastle United kutoka kwa Mike Ashley.
Lakini, Amnesty inachukulia uamuzi wa Saudi Arabia kuwekeza kwenye michezo kama janja ya kuusahaulisha ulimwengu kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na taifa hilo.
“Si jukumu letu kusema nani amiliki Newcastle, lakini wachezaji, wafanyakazi na mashabiki wanatakiwa kujua wanapumbazwa kupitia michezo,” alisema mkuu wa Amnesty, Uingereza, Felix Jakens. “Saudi Arabia imezoea kutumia michezo kama sehemu ya kujitangaza na kuwasahaulisha watu kuhusu uvunjifu wa haki za binadamu katika taifa hilo, ndiyo maana si ajabu kusikia wanataka kuinunua Newcastle.”
No comments:
Post a Comment