Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Jailos Haule anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za mauaji ya baba yake mzazi Gerodi Haule (72) mkazi wa Mawengi wilayani Ludewa mkoani Njombe kwa kumpiga na kitu chenye ncha kali
Kamanda wa Polisi mkoani humo Hamis Issah, amesema kuwa tukio hilo limesababishwa na uwepo wa ugomvi wa kifamilia na imani za kishirikina, uliopelekea kutoelewana kati ya baba na mtoto, ambapo mara baada ya mzee huyo kujeruhiwa, alipelekwa hospitali na baadaye kufariki baada ya hali yake kuwa mbaya.
"Kuna mzee mmoja ameuwawa ana umri wa miaka 72, kutokana na kuwepo kwa ugomvi wa kifamilia ulioleta hali ya kutoelewana, kutokana na mtoto mmoja kwenye familia hiyo kugombana na baba yake na kuchukua kitu chenye ncha kali na kumjeruhi mzee wao" amesema Kamanda Issah.
Aidha katika hatua nyingine Kamanda Issa amesema kuwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, zimesababisha watoto wanne kufariki dunia katika nyakati na maeneo tofauti ya Mkoa huo.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment