Search This Blog
Thursday, December 19, 2019
Waziri Jafo kutumia timu ya uchunguzi wa fedha za miradi Nanyumbu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo ameagiza kufanywa uchunguzi wa fedha zote za miradi ya maendeleo wilayani Nanyumbu kufuatia taarifa za ufujaji wa fedha za miradi zilizo elekezwa wilayani humo.
Timu hiyo cha Uchunguzi kutoka TAMISEMI Makao makuu itaanza kazi mara moja ili kujiridhisha juu ya tuhuma hizo ili endapo itabainika kwamba zina ukweli hatua mbalimbali ziweze kuchukuliwa.
Jafo alitoa maelekezo hayo alipokuwa wilayani Nanyumbu wakati kuanza ziara ya kikazi Mkoani Mtwara.
Wakati huo huo Jafo amefanya ziara wilayani Masasi na kufanya ukaguzi wa ujenzi wa shule ya mfano ya Kisasa ujenzi wa kituo cha Afya Chihungutwa, pamoja na ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya masasi.
Katika ukaguzi huo Jafo amechukizwa sana na wizi wa vifaa vya ujenzi uliofanywa na wananchi katika kituo cha Afya Chihungutwa na ameagiza wananchi hao kukamilisha ujenzi huo kwa fedha zao wenyewe kwani serikali ilishapeleka shilingi milion 400 hivyo haita endekeza tabia za baadhi ya watu wanaoleta masihara katika maendeleo.
Aidha, Jafo amempongeza mbunge wa Lulindi Mhe. Dismas Bwanausi kwa kujituma kwake katika kuwapambani wananchi wake katika maendeleo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment