Search This Blog

Thursday, December 19, 2019

Cristiano Ronaldo aacha watu vinywawazi kwa muda aliokaa hewani na kufunga bao la kichwa



Mchezaji hatari wa klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo aliwaacha wadau, mashabiki na wapenzi wa soka ulimwenguni vinywa wazi baada ya kufunga bao hatari na lililozua gumzo mitandaoni kwenye ushindi waliyopata wa magoli 2 – 1 dhidi ya Sampdoria Jumatano usiku.

Ronaldo akifunga bao hilo dakika 45 za kipindi cha kwanza kupitia kichwa, na kuzua gumzo kutokana na umbali alioruka hewani mpaka kuupata mpira.

Kocha wa timu pinzani, Claudio Ranieri alikaririwa akisema kuwa kwenda hewani kule na kuchukua muda mrefu mpaka kurudi chini ni 'Style za NBA' akimaanisha ndiyo wachezaji pekee wanao ruka juu mno wakati wakitaka kuingiza mpira wavuni.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 34, kupitia bao hilo anafikisha jumla ya magoli 10 akiwa wa pili kwenye mbio za kuwania ufungaji bora Serie A nyuma ya Ciro Immobile mwenye magoli 17.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...