Search This Blog

Sunday, December 15, 2019

Wabunge wa Tanzania wazoa medali lukuki katika michuano ya Mabunge Uganda


Wabunge wanawake kutoka Timu ya Bunge 'Bunge SC' Anatropia Teonest, Rose Tweve, Ester Matiko, Yosepher Komba na Kiongozi wao Naibu Spika, Dk.Tulia Akson wamezoa medali lukuki za dhahabu, Shaba na Fedha katika michuano ya Mabunge inayoendelwa Jijini Uganda.

Wabunge hao wakali wa kufukuza upepo unaweza sema hawaachi kitu, wao wanazoa kila medali hapa Kampala kuanzia kutembea kwa kasi mpaka kukimbia mita 100 mpaka 1500.

Aliyeanza kuing'arisha nyota ya vijana haonwa Ndugai ni mwanadada Rose Tweve aliyeshinda mbio za mita 100 akazoa dhahabu, akaja Yosepher Komba akazoa dhahabu mita 1500 na Anatropia Teonest akazoa Fedha, akaja kwenye mita 400 akazoa tena Fedha.

Hapo jana Mama Lao Dkt Tulia Ackson akazoa dhahabu Kama zote kwenye kutembea kwa kasi. Anatropia Teonest tena kwenye mita 800 akazoa dhahabu na Yosepher Komba akatwaa Fedha Kama zote.

Mita 400 Ester Matiko akazoa Fedha na Rose Tweve akamalizia na Shaba.

Ukaja wakati wa kupokezana vijiti, Aaaah dhahabu Kama zote, mpaka Wakenya wakazungukwa. Alianza Anatropia Teonest, akampasia kijiti Rose Tweve, kisha Ester Matiko akapokea na kumkabidhi Yosepher Komba, hapakubaki kitu, ikawa tena dhahabu Kama zote.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...