Search This Blog
Sunday, December 15, 2019
Serikali yabainisha fursa ya ufugaji samaki ukanda wa Pwani
Serikali imesema inahakikisha sera yake ya kuhamasisha wananchi kufuga samaki inatekelezwa kote nchini ili kutosheleza mahitaji ya soko la samaki nchini pamoja na kukuza pato la taifa na mtu mmoja mmoja.
Akizungumza Mjini Mtwara, wakati akifungua tawi la Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Kampasi ya Mikindani Mkoani Mtwara, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ameiagiza FETA kwa kushirikiana na Idara ya Ukuzaji Viumbe kwenye Maji kutoka katika wizara hiyo, kuandaa mitaala ya ufugaji viumbe kwenye maji wakiwemo samaki, kaa, majongoo bahari na Kambakochi kwa ajili ya wananchi wa Ukanda wa Pwani ili waweze kuongeza vipato vyao kupitia fursa ya ufugaji.
Aidha Ulega ameagiza uundwaji wa vikundi vya uzalishaji kaa, Kambakochi, majongoo bahari pamoja na wazalishaji wa zao la mwani ili iwe rahisi kwa vikundi hivyo kutambulika rasmi pindi mazao yao yanapohitajika sokoni, na watu waweze kufika katika mashamba yao ya ufugaji kwa ajili ya kuvua samaki na viumbe vingine wakiwemo kaa, kambakochi na majongoo bahari ambao wamekuwa na soko kubwa sana na mahitaji yake kuongezeka katika baadhi ya maeneo zikiwemo hoteli za kitalii.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka FETA, Ambakisye Simtoe amesema chuo hicho kimepanga kuzalisha wagani kwa ajili ya kuendeleza na kukuza tasnia ya uvuvi nchini pamoja na kununua mashine ya kuzalisha vifaranga bora ili iwe rahisi kwa wananchi wa Ukanda wa Pwani kupata vifaranga hivyo kwa bei nafuu huku katika risala ya wanafunzi hao wakisema mafunzo waliyoyapata yakiwemo ya ufugaji wa samaki yatawawezesha kujiajiri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment