Search This Blog

Monday, December 9, 2019

Volkano Yalipuka Kisiwani..Mmoja Afariki na Wengine 27 Hawajulikani Walipo Mpaka sasa

New Zealand
Watu 23 wameokolewa huku Polisi ikitahadharisha uwezekano wa kuongezeka kwa vifo katika tukio hilo lililotokea muda mfupi baada ya Watalii kuonekana karibu na mlima huo

Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Jacinda Ardern amesema oparesheni za kuwatafuta manusura zimeanza lakini moshi mkali katika eneo hilo unazuia juhudi hizo

Mlima uliolipuka volkano upo katika Kisiwa kijulikanacho kama 'White Island' maarufu "Whakaari" ikiwa ni moja ya maeneo yenye milima mingi yenye volkano

Licha ya hivyo, Kisiwa hicho huwavutia Watalii ambao huzuru mara kwa mara nyakati za mchana kutokana na kuwepo kwa ndege zinazoendesha shughuli za kitalii

Desemba 3, 2019 Wanajiolojia walitahadharisha kuwa mlima huo huenda ukalipuka kupita kawaida yake, japo waliongeza kuwa kiwango hicho cha mlipuko hakiwezi kuhatarisha maisha ya Watalii

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...