Search This Blog

Monday, December 9, 2019

Mbeya: Auawa Akituhumiwa Kuwatesa Wananchi Kwa Uchawi


Jeshi la Polisi linawashikilia Watu watatu wakidaiwa kumuua John Mwakarundwa(62), Mkazi wa Kijiji cha Nkunga Wilayani Rungwe tukio ambalo linahusishwa na imani za kishirikina

Kamanda wa Polisi Mbeya Ulrich Matei amesema, Mwakarunda alikuwa anatuhumiwa kununua uchawi Malawi hivyo Wananchi wa eneo hilo walikuwa na hasira nae wakidai anawatesa

Amesema, Watuhumiwa walimvamia Mwakarundwa na kumkatakata na vitu vyenye ncha kali maeneo ya kisogoni, taya la kushoto na tumboni

RPC amebainisha, "Watuhumiwa wanadai wamefanya hivyo ili kulipiza kisasi na baada ya kuuawa kwake Wananchi walikuwa wanashangilia wakifurahia kifo chake."

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...