Search This Blog
Monday, December 16, 2019
TMDA yajidhatiti kuongeza uchunguzi wa sampuli
Katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa madarakani, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ya kanda za nyanda za juu kusini imefanikiwa kupima sampuli za dawa mbalimbali zipatazo 744 na dawa moja kati ya dawa hizo ilikutwa ni bandia na ikaondolewa sokoni.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa TMDA kanda ya nyanda za juu kusini Bi. Grace Kapande wakati akiongea na Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Wizara ya Afya na Taasisi zake ambao wametembelea Mkoani Mbeya katika kutekeleza kampeni ya
“Tumeboresha Sekta ya Afya yenye lengo la kuuhabarisha umma kuhusiana na maboresho makubwa yaliyofanyika katika Sekta ya afya kwa kipindi cha miaka minne," amesema.
Bi. Grace amesema TMDA imefanikiwa kuongeza ufanisi kwa kununua maabara mbili zinazohamishika katika mikoa ya Rukwa na Songwe zinazofanya uchunguzi na kutoa viashiria vya awali ambavyo si salama kwa dawa husika na hivyo kusafirisha sampuli hiyo kwenda kwenye maabara kuu iliyoko jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kaimu Mkurugenzi huyo amesema kuongezeka kwa maabara hizo kumesaidia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa idadi ya sampuli zinazopimwa katika maabara mbalimbali za Mikoa ya nyanda za juu kusini na zinatoa taarifa kila mwezi hivyo kuongeza ufanisi wa mamlaka hiyo.
TMDA kanda ya nyanda za juu kusini inahudumia mikoa mitano ambayo ni Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe na Rukwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment