Search This Blog
Monday, December 16, 2019
Cristiano Ronaldo akataa kuvaa kitambaa cha unaodha, kisa?
Mshambuliaji wa Juventus ya Italia Cristiano Ronaldo amekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii kufuatia uamuzi wake wa kukataa kuvaa kitambaa cha unaodha katika mchezo wa Juventus dhidi ya Udenise wa Ligi Kuu ya nchini Italia (Serie A), waliopata ushindi wa 3-1 na kuifikia Inter Milan kwa kuwa nao sawa kwa point 39 ila Inter ikiongoza kwa tofauti ya magoli.
Kitambaa cha unahodha katika mchezo huo kilivaliwa na Leonardo Bonucci lakini baada ya kufanyiwa mabadiliko akampa kitambaa hicho Gonzalo Higuan ambaye nae dakika 5 baadae akatolewa ndipo akaenda kumpatia kitambaa cha unahodha Cristiano Ronaldo na kukikataa.
Ronaldo alikichukua kitambaa hicho na kwenda kumvalisha mchezaji mwenzake Blaise Matuidi kama heshima kutokana na mchezaji huyo kucheza Juventus kwa muda mrefu, hivyo inadaiwa Ronaldo hakuona kama anastahili kuvaa kitambaa mbele ya Blaise Matuidi aliyemkuta katika club hiyo wakipishana mwaka mmoja (Ronaldo 2018, Matuidi 2017 akitokea PSG)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment