
KOCHA mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ameonyesha dhahiri kwamba anahitaji Kombe la Carabao baada ya kusema hawana cha kupoteza kwenye mchezo wao dhidi ya Colchester.
Solskjaer anaona kwamba kushinda taji hilo msimu huu ni muhimu kwa sasa kwa wachezaji waliopo hasa kwa kuanzia mchezo wa kesho Jumatano wa robo fainali dhidi ya Colchester.
Kocha huyo amesema anayachukulia mashindano hayo kwa umakini na kwa msisitizo kwa kuweka timu imara kama ambayo ilicheza na Chelsea katika mchezo uliopita.
"Tutawaonyesha kwa timu ambayo tuliiweka katika mchezo wetu dhidi ya Chelsea, japo tuna wakati mgumu kwenye ligi lakini kuna umuhimu kwa kutengeneza wakati mzuri na kuwaamini waamini wachezaji, naamini tunafika fainali,"
"Naamini kabisa timu ambayo naiandaa itaenda kuwa timu nzuri vyakutosha na kushinda mchezo huu," alisema.
Aliongeza kwa kusema kitu kikubwa ni kutengeneza nafasi za kutosha ili kuweza kupata magoli ambayo yatawasaidia katika mchezo huo.
No comments:
Post a Comment