Search This Blog

Friday, December 13, 2019

Ronaldo awataka Madrid fainali

TURIN, ITALIA . SUPASTAA wa Juventus, Cristiano Ronaldo amesema atapenda sana kuvaana na timu yake ya zamani ya Real Madrid kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
Straika huyo Mreno aliisaidia Madrid kubeba mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ndani ya miaka mitano, lakini aliachana na timu hiyo kwenda zake kujiunga na Juventus.

Na sasa Ronaldo anaweza kuchuana na waajiri wake wa zamani kwenye hatua ya 16 ya michuano hiyo msimu huu baada ya Juventus kumaliza vinara kwenye kundi lao la Madrid wanaoonolewa na Zinedine Zidane kumaliza nafasi ya pili kwenye kundi.
Akitambua hilo kuwa na uwezekano wa kutokea, Ronaldo alisema kitu ambacho atapenda kama atakutana na waajiri wake hao kwenye mchezo wa fainali utakaopigwa huko Uturuki.
"Real Madrid ni timu nzuri, lakini ningependa kukutana nao huko mbele," alisema Ronaldo.
“Fainali? Ningependa sana kukutana nao  kwenye mchezo wa fainali.”

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...