Search This Blog

Monday, December 23, 2019

Real Madrid yampeleka Isco Chelsea

London, England. Chelsea italazimika kutoa Pauni44 milioni kupata saini ya mchezaji wa kiungo wa Real Madrid Isco katika usajili wa dirisha dogo.

Real Madrid imemuweka sokoni kiungo huyo ili kutoa nafasi kwa nyota wa Tottenham Hotspurs Christian Eriksen kumsajili mwezi ujao.

Eriksen ameweka bayana dhamira ya kuondoka Spurs tangu msimu uliopita akitaka kujiunga na matajiri hao wa Santiago Berbabeu.

Kocha Frank Lampard wa Chelsea anataka kuimarisha kikosi baada ya kuondolewa adhabu na miongoni mwa wachezaji anaowinda yumo Isco.

Licha ya kutajwa na wachambuzi ni mmoja  wachezaji bora wa viungo, Isco (27)  hana namba mbele ya kocha Zinedine Zidane.

 Lampard ana Pauni150 milioni za usajili anazotarajiwa kutumia katika dirisha dogo, hivyo Isco anaweza kuingia katika mtego wa fedha hizo.

Advertisement

Pia Real Madrid inaweza kuwapiga bei Gareth Bale na James Rodriguez endapo itakidhi vigezo vya kiwango cha fedha zilizowekwa na Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa).

Klabu hiyo inatakiwa isivuke lengo la matumizi ya fedha zilizowekwa na Uefa baada ya msimu uliopita wa majira ya kiangazi kutumia Pauni295 milioni kuwasajili Eden Hazard na Luka Jovic.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...