Search This Blog
Sunday, December 29, 2019
Polisi Arusha wafanikiwa kumkamata aliyemuua mkewe kwa shoka
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa Moses Pallangyo (28), aliyemuua mwanamke aliyekuwa akiishi naye Mary Mushi kwa kumkata na shoka kichwani, katika Kijiji cha Kilinga wilayani Arumeru na baada ya mahojiano, mtuhumiwa huyo amekiri kufanya mauaji hayo.
Akizungumza jana, Jumapili Disemba 29, Kamanda wa Polisi mkoani humo Jonathan Shanna, amesema kuwa jeshi hilo lilimsaka mhalifu huyo kwa kutumia Kikosi cha Mbwa ambacho ndicho kilichofanikisha kumkamata, akiwa mafichoni kuelekea nchini Kenya.
"Jana Disemba 28 saa 11: 30 jioni, tulifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo, ambaye tuliahidi kumtafuta kwa namna yoyote ile na 'Dog Style' ndiyo imeleta mafanikio ya kumkamata yaani ilikuwa bandika bandua, mtuhumiwa tumemhoji kwa kina na amekiri kufanya kitendo hicho cha kikatili, na tulitaka kujua sababu ya kufanya kitendo hicho amesema ni shetani alimpitia," amesema Kamanda Shanna.
Tukio la mauaji hayo lilitokea Disemba 25, wilayani Arumeru jambo ambalo awali lilihusishwa na ugomvi wa kifamilia ikiwemo wivu wa mapenzi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment