
HABARI ndiyo hiyo. Real Madrid wameripotiwa kwamba wapo tayari kuwapa Manchester United fursa ya kuwachukua Gareth Bale na James Rodriguez ili wabadilishane na Paul Pogba.
Kiungo huyo Mfaransa, Pogba amekuwa nje ya uwanja akiripotiwa kwamba hajapona vizuri, lakini siku za karibuni kocha wa Manchester, Ole Gunnar Solskjaer amesisitiza mpango wa kuachana na staa huyo kwenye dirisha la Januari.
Kwa mujibu wa El Desmarque, Real Madrid wanataka kuchukua nafasi hiyo kama sehemu ya kuwashawishi Man United ili wao wamchukue Pogba.
Mastaa hao wawili wanaonekana si kitu huko Bernabeu, lakini watakapotua Old Trafford watapata nafasi kikosi cha kwanza kama dili hilo litafanyika kwenye dirisha la Januari. Lakini, shida ni kwamba Man United wanang’ang’ania kupewa pesa kwenye dili linalomhusisha kiungo huyo ambayo amebakiza miaka miwili na nusu huko Old Trafford.
Pogba amekuwa akihusishwa pia kurejea Juventus, klabu yake aliyotokea kutua United.
No comments:
Post a Comment