Search This Blog

Monday, December 16, 2019

Mwamnyeto ampania Okello

By Charles Abel

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Uganda, Allan Okello amekuwa gumzo katika mashindano ya Chalenji yanayoendelea jijini hapa, lakini hilo limeonekana kutowapa hofu mabeki wa timu ya Taifa ya Bara, Kilimanjaro Stars’ ambao leo Jumanne watakabiliana naye katika mechi ya nusu fainali itakayochezwa kwenye Uwanja wa KCCA.

Beki wa Kili Stars, Bakari Mwamnyeto alisema yeye na mabeki wenzake wanafahamu ubora wa Okello mwenye umri wa miaka 19 ambaye anachezea KCCA lakini wamejipanga vyema kuhakikisha haleti madhara langoni mwao.

“Yupo yule mshambuliaji wao anayetumia mguu wa kushoto (Okello) ni mzuri na msumbufu lakini tumejipanga kumkabili vya kutosha.

“Tunatakiwa kuziba nafasi ili wasipate mwanya wa kufunga au kumsogelea kipa wetu. Nina imani tukifanya hivyo, tutakuwa na nafasi kubwa ya kupata ushindi,” alisema Mwamnyeto.

Jina la Okello limekuwa maarufu nchini Uganda kutokana na kiwango bora ambacho amekuwa akikionyesha ndani ya jezi ya timu ya taifa ya nchi hiyo na timu yake ya KCCA.

Katika mashindano ya Chalenji, Okello amepachika mabao mawili na kuchangia kupiga pasi za mwisho zilizozaa mabao matatu na amekuwa akipewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mashindano hayo.

Advertisement

Lakini kama hilo halitoshi, juzi Jumamosi usiku, Okello aliibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Uganda wa mwaka ambapo alipatiwa kitita cha Sh 1 milioni za Uganda na gari.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...