Mfanyabiashara nchini Tanzania, Maiko Mrina (67) na wenzake wawili wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwamo la kuisababishia Serikali ya Tanzania hasara ya Sh30 milioni na kuiba nondo tani nane.
Mbali na Mrina, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni ya uhujumu uchumi namba 140/2019 ni dereva, Ally Athumani (36) mkazi wa Mbagala na mlinzi Shabani Rashidi (57) mkazi wa Mwananyamala wote wa jijini Dar es Salaam.
Katika kesi hiyo, Mrina amesomewa mashitaka yake hospitalini leo Jumanne Desemba 24, 2019 akiwa amelazwa wodi namba mbili katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) baada ya kuugua.
Washitakiwa hao walisomewa mashtaka na jopo la mawakili watatu wa upande wa mashtaka, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Vicky Mwaikambo.
Wakili wa Serikali Mkuu Mkunde Mshanga akisaidiana na wakili wa Serikali mwandamizi Wankyo Simon na Grory Mwenda, washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo kati Agosti 29 na 30, 2018 katika eneo la Ubungo.

No comments:
Post a Comment