Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jana 24 Disemba 2019 amehudhuria na kushiriki mazishi ya Mama mzazi wa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Innocent Kalogeris
Mama Theodora Vasos Kalogeris amefariki dunia Jumapili 22 Disemba 2019 Hospital ya Chuo cha Kilimo (SUA) Morogoro na kuzikwa jana alasiri makaburi ya Kola Hill Morogoro Mjini.
Mapema viongozi na wanachama walipata kuaga mwili kisha kufanyiwa ibada fupi nyumbani kwake Mji mpya na baadae kufuatiwa na Ibada ya mazishi kanisa la Kuu St Patrick.
Viongozi wengine walishiriki Mazishi hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Katibu Mkuu wa UWT, Wabunge kutoka mkoa wa Morogoro na Mbunge wa jimbo la Korogwe Marry Chatanda, Wakuu wa Wilaya zote za mkoa huo, IGP mstaafu Mahita, Mwenyeviti wa Chama wa Wilaya zote wakiongoza kamati za siasa za Wilaya zao, wakuu wa vyombo vya ulinzi na ulinzi na Usalama mkoa huo, wakuu wa taasisi za umma pamoja na ndugu jamaa na marafiki.

No comments:
Post a Comment