Search This Blog

Wednesday, December 4, 2019

Kampuni yaja na mbinu mbadala kutangaza utalii wa ndani


Katika harakati za kufanikisha mpango wa kuendeleza utalii wa ndani (Domestic Tourism Promotion Initiative - DTPI) unaotarajiwa kufanyika mikoa mbalimbali nchi nzima, Kampuni ya Real PR Solutions ya jijini Dar es Salaam, imeandaa tamasha linalojulikana kama ‘Twenzetu Kilimanjaro Fest’ 2019, litakalofanyika tarehe 22 Disemba 2019 katika viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi.

Tamasha hilo litahusisha agenda kuu tatu ambazo ni pamoja na kutangaza utalii wa ndani, upandaji wa miti pamoja na kuhamasisha uwekezaji wa viwanda katika mkoa huo.

Tamasha hili linatarajiwa kupambwa na matukio kadhaa ya burudani zikiwemo, Mbio za kujifurahisha za Capital Mountain Run zitakazohusisha Km 5, Km 10 pamoja na mbio za watoto za Km 3 na Mbio za Baiskeli za KM 60, Maonesho ya Utalii na Biashara, Burudani na viburudisho mbalimbali ikiwemo michezo ya watoto, vyakula vya asili na muziki.

Aidha katika mkakati wake wa kufanikisha agenda hizo, kampuni hiyo imeandaa matukio kadhaa ya kijamii ili kuunganisha wadau mbalimbali wa mkoa huo kama vile utembeleaji wa vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo mkoani Kilimanjaro ikiwemo, Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi na maporomoko mbalimbali ya maji yaliyopo mkoani humo.

“Tutukio hili la utembeleaji wa vivutio na upandaji miti linatarajiwa kufanyika Disemba 21, 2019 yaani siku moja kabla ya Tamasha,’’ amesema Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo Clement Mshana.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...