Search This Blog
Sunday, December 22, 2019
Bondia Kyotaro Fujimoto ashindwa kuhimili nguvu za Daniel Dubois
Bondia Muingereza wa uzito wa juu Daniel Dubois ameendeleza rikodi yake ya kutopigwa katika ushindi mtamu wa knockout (KO) dhidi ya Kyotaro Fujimoto katika uwanja wa ndondi wa ndani wa London Copper Box.
Dubois, mwenye miaka 22, amepewa nafasi kubwa ya kujitokeza kama mshindani wa taji la ulimwengu na kumtawala mpinzani wake Mjapani, akimlaza sakafuni katika raundi ya pili.
Fujimoto alifanikiwa kujizoa sakafuni lakini kipigo kikali alichokipata baada ya hapo kilimfanya ahitaji matibabu.
Fujimoto alishinda mapambano 21 kati ya mapambano yake 22 ya nyumbani lakini pambano lake la kwanza nje ya Japan lilionekana kumchosha mbele ya jitu la miraba saba.
Dubois sasa amewashinda wapinzani wake 13 kati ya 14 na promota wake Frank Warren amekuwa akiongea kuhusu kumsongesha mbele katika nafasi ya lazima ya kuwania taji la dunia mwaka 2020.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment