
LONDON, ENGLAND . MIKEL Arteta amekubali kujiunga Arsenal na sasa yupo tayari kupiga kazi, lakini kuna staa wa zamani wa timu hiyo amemtajia wachezaji watano ambao anapaswa kuwapiga chini kuweka mambo sawa Emirates.
Kwa miaka mitatu iliyopita, Mhispaniola huyo alifanyakazi akiwa msaidizi wa Pep Guardiola kwenye kikosi cha Manchester City na amekuwa akipambana na presha zote katika kuifikisha timu hiyo kwenye mafanikio makubwa. Sasa anakwenda Arsenal, mahali ambako atakuwa kwenye presha kubwa zaidi kutokana na timu hiyo kushika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England kwa sasa.
Kazi yake ya kwanza Arteta huko Arsenal itakuwa kurudisha morali kwenye vyumba vyua kubadilishia, hilo linaendana na kuondoa wachezaji ambao hawapo tayari kuendelea kubaki klabuni hapo.
Staa wa zamani wa Chelsea na Marseille, Tony Cascarino amemtajia Arteta wachezaji watano ambao anapaswa kuwaondoa haraka kwenye timu.
Alisema: "Changamoto kubwa inayomkabili kuwahimili wachezaji wakubwa kwenye timu. Nakumbuka Ron Atkinson alipokuja Aston Villa, alikuja moja kwa moja kwangu na kuniambi: 'Nimeshakubaliana na Celtic kuhusu wewe.' Hivyo ndivyo Arteta anapaswa kufanya, aanzie na Pierre-Emerick Aubameyang, Alexandre Lacazette, David Luiz, Mesut Ozil na Shkodran Mustafi."
Ukiacha mastaa wa kuwaondoa, Cascarino amemwambia Arteta wachezaji wa kuwachukua akiwamo kiungo wa Man City, Fernandinho hasa kwa kipindi hiki ambacho Mbrazili huyo mkataba wake huko Etihad unafika tamati mwisho wa msimu. Wachezaji wengine anaotaka awasajili ni Wilfried Zaha na Dayot Upamecano.
No comments:
Post a Comment