Search This Blog

Thursday, December 19, 2019

Arteta abebeshwa zigo la Pierre Emerick Aubameyang Arsenal

MABOSI wa Arsenal wanaamini kwamba ujio wa Mikel Arteta kwenye kikosi hicho utamshawishi straika Pierre-Emerick Aubameyang kusaini dili jipya la kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Kaka wa straika huyo, Willy, alisema hadharani kuhusu Arteta kwamba hana uzoefu wa kwenda kuwa kocha wa timu kubwa kama Arsenal. Kauli hiyo imewakera mashabiki wa Arsenal kwa kudai kuwa sio ya kiuungwana.

Aubameyang amebakiza miezi 18 katika mkataba wake huko Arsenal huku mshahara wake akilipwa Pauni 200,000 kwa wiki na hana haraka ya kuongeza dili jipya.

Arsenal haitaki kumwaachia fowadi wake huyo mwenye mabao 13 aondoke, ikiwa ilimnasa kwenye kikosi chake miaka miwili iliyopita akitokea Borussia Dortmund ya Ujeruman kwa ada ya Pauni 56 milioni.

Hata hivyo, Arsenal haina shida hata kama Aubameyang atabaki kwenye timu bila ya kusaini dili jipya na kuondoka bure mwaka 2021 wakati mkataba wake utakapofika tamati.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...