Search This Blog

Wednesday, November 6, 2019

Waziri wa Elimu afanya mazungumzo na Mkuu wa UNICEF nchini


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako hapo jana Novemba 6, 2019 alikutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Elimu Tanzania kutoka Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Tanzania, Dkt. Daniel Baheta.

Dkt. Baheta amefika katika ofisi za Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia zilizopo Jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo ambapo amemweleza waziri kuwa UNICEF inatekeleza vipaumbele vitatu katika sekta ya elimu.

Mkuu huyo amevitaja vipambele vya Kimataifa vya UNICEF kuwa ni kuwa ni ubora katika utoaji elimu na ujifunzaji, elimu kwa vijana, ajira na kutatua changamoto ya mdondoko wa wanafunzi katika shule.

Waziri Nadlichako amesema angependa kuona UNICEF ikishirikiana zaidi na Serikali katika kuimarisha mafunzo ya stadi za maisha ambazo zitawawezesha wanafunzi wa kike kukwepa vishawishi vinavyosababisha mdondoko shuleni na ukuzaji wa ushirikishwaji jamii katika kusimamia ubora wa elimu na wanafunzi.

Katika mazungumzo yao wamekubaliana kutekeleza programu ambazo ni pamoja na kuanzisha mfumo wa kidigitali wa kusimamia mahudhurio ya wanafunzi na kuwezesha mawasiliano kati ya Taasisi za elimu na wazazi.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...