Search This Blog

Monday, November 25, 2019

Usipime makocha wanawake waliotikisa Cecafa

By Doris Maliyaga

MCHEZO wa soka kwa wanawake katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati umepiga hatua kubwa na hii imejionyesha kwenye michuano ya Cecafa iliyomalizika jana Jumatatu Chamazi, Dar es Salaam.

Kwani kati ya makocha wakuu wanane walioongoza timu hizo watatu ni wanawake. Makocha hao ni Mfaransa M’barek Sarah wa Djibouti, Faridah Belega wa Uganda na Niyibimenya Daniella wa Burundi.

Makocha hao hakuwa na tofauti ya jinsia kwani kati yao wawili, Faridah wa Uganda na Daniella wa Burundi walizipeleka timu zao hatua ya nusu fainali.

Mbali na Burundi na Uganda zilizoingia nusu fainali, Kenya inayonolewa na David Ouma na wenyeji Tanzania Bakary Shime, zilikutana fainali.

M’BAREK SARAH (DJIBOUTI)

Kocha Mkuu wa Djibouti, M’barek Sarah hana muda mwingi tangu ajiunge na timu hiyo, mpaka anashiriki michuano ya Cecafa alikuwa na miezi miwili tu.

Advertisement

Kiungo huyo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Ufaransa mwenye umri wa miaka 42, ana Leseni A ya Uefa. Alizichezea timu za vijana za Vallee du Lyspont, Orleans, Touraine na La Roche-Sur-Yon

Klabu La Roche-Sur-Yon ilimpandisha timu ya wakubwa msimu wa 2000-2001, mwaka uliofata Montpelier ilimchukua akacheza hadi 2007, alipopewa ukocha.

Akiwa kocha mbali na kuifundisha Montpellier aliinoa pia Guingamp aliyoachana nayo mwaka huu akajiunga Djibouti.

Sarah aliyezaliwa Chamontifram mwenye urefu wa futi 5 na nchi 7, anasema: “Nimeyefurahia mashindano kwa sababu vijana wanajifunza na nimeshangaa kuona soka la Afrika linakuwa kwa kasi kiasi hicho kutokana na kiwango kikubwa kilichoonyeshwa. “

“Timu yetu inashiriki kwa mara ya kwanza lakini tunaondoka na kitu kiasi kwamba tukija kwa mara nyingine tutakuwa watu tofauti kutokana na tulivyojifunza,” anasema Sarah.

Awesome aliongeza: “Tumejipa miaka miwili ya kutengeneza timu na baada ndipo tutakuwa na cha kuzungumza.”

NIYIBIMANYA DANIELLA (BURUNDI)

Kwa mwonekano unaweza kumchukulia poa, Kocha Niyibimanya Daniella, mbona dogo tu, hawezi kujua soka huyu, lakini kumbe kichwani kuna ufundi, mbinu na mipango kibao.

Ana Leseni A ya CAF na ameipata baada ya kuhenyeka na makocha wakubwa wanaume kama Etienne Ndayiragije wa Taifa Stars na Masoud Djuma aliyeinoa Simba miaka ya nyuma.

“Katika darasa Leseni A, mwanamke nilikuwa peke yangu. Ndiye mwenye Leseni A, Burundi wengi waliofanikiwa wana C,” alisema Niyibimanya aliyepata Leseni A, B wakati D na C alipata ndani ya mwaka 2012 alikuwa bado anacheza soka.

“Nimesoma darasa moja na Étienne, Masoud ndio mwanamke nilikuwa mimi tu na nina uzoefu wa kuucheza mpira, nimecheza kwa miaka 13.”

Mchezaji huyo wa zamani wa Lokolombe ya Burundi anasema, kuchaguliwa kuifundisha Timu ya Taifa ya Burundi ya Wanawake, walifanya mtihani makocha wanane kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo vyuoni akachaguliwa yeye.

“Ulikuwa mtihani wa darasani na vitendo kifundisha, mwisho nikapita mimi.”

Anasema, ana uzoefu wa kufundisha timu za kiume pia, aliifundisha Inter Club akiwa msaidizi wa Masoud Juma na anafafanua tofauti zao.

“Mtoto wa kiume anafaida kubwa katika mchezo huu kwa sababu hana majukumu mengi nyumbani. Mtoto wa kiume yuko tayari muda wote ukimweka uwanjani anacheza, ustahimilivu wa mwili na pumzi inakuwepo,” anasema Daniella.

“Lakini, wa kike anahitaji maandalizi ya muda mrefu mnapokuwa na mashindano kama haya kwa sababu anakuwa hayuko tayari kwa mazoezi kutokana na majukumu mengi aliyonayo nyumbani, anakuwa mtoro wa mazoezi.”

Anasema, ni kiongozi wa ufundi kwenye shirikisho lao la Burundi, anakwenda sehemu mbalimbali ndani ya nchi hiyo kwa ajili ya kutafuta vipaji vya soka.

Kuhusu mashindanoya Cecafa, Daniella ambaye malengo ya mwaka huu yalikuwa ni kuingia nusu fainali nafasi ambayo wameipa anasema : “Mashindano yamekuwa mazuri, vipaji vimeonekana. yanatakiwa kufanyika mara kwa mara.”

FARIDAH BELEGA (UGANDA)

Kocha Mkuu wa Uganda, Faridah Belega amezaliwa miaka 30, iliyopita kwao, Uganda. Ana Leseni B ya CAF na tangu aanze ukocha huu ni mwaka wa tano.

Mbali na kuinoa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Uganda huu ukiwa ni mwaka wa pili pia, anaifundisha Klabu ya Kampala United kwa sasa inayoshiriki mashindano Uganda.

Kocha huyo, alicheza mpira tangu akiwa mdogo shule za msingi, aliendelea hivyo akacheza mpira wa ushindani 2001 hadi 2010 alipostaafu.

Alizichezea Klabu za Kampala United na Haerts United ambazo zinacheza mpira wa ushindani.

Anasema: “Mashindano yalikuwa na ushindani mkali, timu zimeonyesha viwango vya juu na ushindani.”

“Mawazo yangu kwa miaka ijayo kuna mambo yanatakiwa kufanyiwa kazi hasa ya kiofisi. Waamuzi kwa kiasi fulani hawakuwa vizuri kwa asilimia zote kuna mambo mengine yalikuwa hayaendi sawa,” anasema Faridah.

WASAIDIZI WANAWAKE KAMA WOTE

Mbali na makocha hao wakuu, timu za taifa za wanawake zilikuwa na makocha wengi wasaidizi wanawake ambao ni

Tanzania Bara alikuwepo, Edna Lema, Ethiopia ilikuwa na Maruta Meseret, Burundi msaidizi wake aliwakuwa, Ininahazwe Belyse na Timu ya Kenya iliyofahamika mama Harambee Stralets ilikuwa na Jacqueline Juma.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...